09/05/2025
Ungependa kushiriki session ya Ugali Elimu 10/05/2025? Wasiliana nasi kwa 0747981275 kwa ajili ya utaratibu.
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Ugali Elimu, Education, Kapina Close, Dar es Salaam.
Kuinua jamii kupitia kilimo endelevu, kukuza ujuzi wa matumizi ya vyakula vya asili kudhibiti matatizo ya utapiamlo kwa kushirikisha maarifa ya mlo bora sahihi.
09/05/2025
Ungependa kushiriki session ya Ugali Elimu 10/05/2025? Wasiliana nasi kwa 0747981275 kwa ajili ya utaratibu.
26/04/2025
Ugali Elimu Hapa tunapata Elimu ya Umuhimu wa makundi sita ya chakula. Mtalaamu ni Ms Maria Ngirisho kutoka Mamlaka ya Lisha na chakula Tanzania TFNC Tanzania
26/04/2025
Ugali Elimu Darasani hapa tupo na Mzee wetu Dr Albinus Makalle akitupa Madini kwenye eneo la ujasiriamali. Hapa ni Malembo Farm HQ
ll ll
26/04/2025
Ugali Elimu ni kila jumamosi hapa Malembo Farm HQ.
11/04/2025
Kesho ni siku nyingine tena ya Ugali Elimu , Malembo Farm HQ. ungependa kushiriki wasiliana nasi kwa 0747981275
**aChakula
08/04/2025
Leo Mkurugenzi mtendaji wa Malembo Farm Ndugu Malembo Lucas akiwakilisha asasi ya kijamii ya Ugali Elimu . Amefanya mazungumzo Mkurugenzi Lishe,Elimu na mafunzo wa Mamlaka ya chakula Tanzania TFNC Tanzania Dr Esther J. Nkuba (PhD)
Mazungumzo hayo yalikuwa ni kuangazia juu ya shughuli zinazofanywa na asasi ya kijamii ya Ugali Elimu.
06/04/2025
Ugali Elimu Powered by Malembo Farm
09/07/2024
Abroad✈️.
here at Frederiksberg, Copenhagen, Denmark. Uniting in this corner of the world by having a healthy dinner and great conversation. shout out to for inspiration.
11/06/2024
Vyakula vya nafaka nzima na nafaka zilizoprocessed zinatofauti katika muundo wao na jinsi zinavyoathiri mmeng'enyo wa chakula na mwili:
1. Muundo;
✅Vyakula vya Nafaka Nzima: Hivi vyenye ganda la nafaka zima, pamoja na utando, kiini, na endospermu. Hii inamaanisha kuwa vina virutubisho vyote na nyuzinyuzi bila kuharibika.
✅Nafaka zilizoprocessed: Nafaka hizi, k**a vile mchele mweupe au mkate mweupe, zimeondolewa utando na kiini wakati wa usindikaji, zikibaki hasa na endospermu yenye wanga.
2. Mmeng'enyo;
✅Vyakula vya Nafaka Nzima: Uwepo wa utando na nyuzinyuzi katika nafaka nzima unapunguza kasi ya mmeng'enyo wa chakula. Hii husababisha kutolewa kwa glukosi mwilini kwa polepole, kuzuia kuongezeka haraka kwa viwango vya sukari kwenye damu.
✅Nafaka zilizoprocessed: Nafaka zilizoprocessed kawaida humeng’enywa kwa haraka, na kusababisha kuongezeka kwa haraka kwa viwango vya sukari kwenye damu.
3. Yaliyomo kwa Virutubisho;
✅Vyakula vya Nafaka Nzima: Nafaka nzima ni tajiri katika virutubisho k**a nyuzinyuzi, vitamini, madini, na antioxidants. Hutoa nishati endelevu, kuchochea afya ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, na kutoa faida mbalimbali za kiafya.
✅Nafaka zilizoprocessed: Nafaka zilizoprocessed hupoteza virutubisho vingi wakati wa usindikaji, ikisababisha thamani ndogo ya lishe.
4. Athari kwa Afya;
✅Vyakula vya Nafaka Nzima: Kula nafaka nzima kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa sugu k**a ugonjwa wa moyo, kisukari cha aina ya pili, na baadhi ya saratani. Pia husaidia katika kudhibiti uzito.
✅Nafaka zilizoprocessed: Lishe yenye kiwango kikubwa cha nafaka zilizoprocessed inahusishwa na ongezeko la hatari ya matatizo ya afya, ikiwa ni pamoja na kunenepa kupita kiasi na upinzani wa insulini.
Kwa muhtasari, vyakula vya nafaka nzima ni bora zaidi kwa mmeng'enyo wa chakula na afya kwa ujumla kwa sababu vinahifadhi virutubisho vyao asilia na nyuzinyuzi, ambayo husababisha mmeng'enyo wa polepole na udhibiti bora wa sukari kwenye damu.
Nafaka zilizoprocessed, kwa upande mwingine, hazina virutubisho muhimu na zinaweza kusababisha kuongezeka haraka kwa viwango vya sukari kwenye damu wakati zinapotumiwa kwa wingi.
Ni vyema kujumuisha nafaka nzima zaidi katika lishe yako kwa faida bora za afya.
Kila jumamosi tuna marafiki tunakutana tunakula ugali pamoja uku tukipeana Elimu kuhusu chakula,Afya,jamii,kilimo biashara kujua fursa na changamoto zake n.k
Malembo Farm
Malembo Lucas
| 13:30 - 17:30 |