21/09/2025
UMOJA Forums
UMOJA Forum is a social network where we share different ideas on politics~sports and games~family and love affairs~education and business.
21/09/2025
Goodmorning Africa,,,!
Ni asubuhi njema na tulivu. Poleni nyote mnaokumbana na changamoto za maisha na bado hamjapata suluhisho la kudumu la kutatua changamoto hizo. Endelea kumuamini Mungu kwani ni yeye pekee awezae kuyabadili maisha yetu na kutupa kile tunachostahili.
Unafkiri kufanya nini leo? mawazo yako ni yapi? biashara, familia na ndoa, elimu au kuwasaidia wengine ili wafikie malengo yao? Jipe nafasi ya kutafakari kuhusu kile unachokihitaji katika maisha kabla ya kufanya jambo lolote. Weka mipango yako kwenye karatasi na chagua mpango mmoja ambao unaweza kutekelezeka na kisha anza kuufanyia kazi. Fanya mara nyingi uwezavyo ili kupata matokeo chanya.
Katika mapambano yako ya leo, tambua kwamba, kuanguka ni shemu ya mapambano.
Naitwa Delisia, Nina miaka 23 kwa sawa. Nkiri kwamba mpaka nafikia umri huu sijawahi kushuriki tendo LA ndoa na kijana yeyote. Kuna wakati nilitamani hata kuacha masomo kwa sababu nilihisi kila MTU anajua shida ya maumbile yangu.
Ndugu zangu, kupitia page hii naamini nitapata mawazo ya kunisaidia kutoka kwenu. Nina sifa zote kuwa mwanamke. Tatizo langu ni kwamba Nina sehemu ndogo ya kiume ambayo urefu wake ni k**a nchi tatu k**a na nusu. Hii hali inanipa shida sana. Naona shida hata kukutana na mwanaume. Kuna kaka mmoja ananipenda sana lkn naona shida kumueleza juu ya tatizo langu hili.
Naombeni ushauri wenu rafiki zangu nifanyeje maana kuna wakati nakuwa na mawazo sana, nashindwa kujielewa. Nina hisia zote za k**e ila tatizo Nina uume pia.
Asante Admin.
Maisha na mtazamo wa mafanikio
Kwanini tunakuwa na kiu ya mafanikio? Ni kwanini tunapokosa yalio matarajio yetu katika maisha tunakuwa wenye huzuni? Tafakari vizuri maneno ya Vitabu vitakatifu: Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadam na kisha akampatia hati miliki ya vitu vyote duniani, yaani, ikiwemo mimea, wanyama na utajiri wote katika USO wa dunia.!
Pointi yangu ni hii, 'Hatupaswi kuwa masikini kwa sababu si madhumuni ya muumba wetu. Hatupaswi kuwa na taswira ya kushindwa ktk maisha yetu kwa sababu si kusudi la Mwenyezi Mungu kwetu.
Siku ya Leo, chukua muda na utafakari juu ya mambo yanayokukwamisha kufikia malengo yako. Ukisha yatambua, mwambie Mungu kwamba nahitaji kurudishiwa hati miliki ya mali zangu. Na Bwana atatenda!! Barikiwa!!
"...andike chohote unachojua kuhusu maneno haya, "maarifa jumuishi(generalized knowledge) na maarifa mahsusi (specialized knowledge) ".
Nitakueleza kwa kina jinsi ambavyo unaweza kutumia aina hizo mbili za maarifa ili kufikia malengo yako...
02/01/2017
Kheri na fanaka ya mwaka mpya 2017. Bwana mwema aishie milele zote azidi kuwaangazia nuru ya uzima na mafanikio kila uchwao.
Leo, tuangalie mambo machache ya muhimu katika kumchagua mwenzi wa maisha(mchumba).
Ndoa ni taasisi takatifu iliyoanzishwa na mwenyezi Mungu kwa kuwaunganisha mume na mke kuwa mwili mmoja!! Unapo ianza safari ya kumpata mwenzi wako wa maisha tafakari mambo yafuatayo:
1. Dini/imani zinazofanana. Jambo hili ni la msingi sana ktk kujenga ndoa na familia yenye afya kiroho. Kutofautiana ktk imani au dhehebu huleta mtafaruku mkubwa hasa kwa watoto wanapokuwa wamezaliwa. Watoto wanaweza kushindwa kupata sehemu sahihi ya kuabudu endapo baba na mama watakuwa na sehemu tofauti kwa ajili ya ibada.
2. Kiwango cha elimu. Jiridhishe kwamba mtu unae hitaji kuishi nae hamzidiani sana kielimu. Hii ina faida kubwa sana ktk suala la kufanya maamzi ndani ya nyumba hasa ktk masuala ya kipato na maamzi mengine ktk familia. Lakini si lazima kwamba wana ndoa watarajiwa walingane ktk kiwango cha elimu, walengwa wanaweza kukubaliana kuisji pamoja huku wakiweka mipango thabiti ya kusaidiana ili kila mmoja afikie matakwa yake kielimu.
3. Umri. Hakikisha hamuachani mbali sana na mwenzi wako kiumri. Kumbuka, ndoa ni faraja. Mmoja wenu anapokuwa na umri mkubwa sana, wakati mwingine inaweza kuwa ngumu ktk kutimiza yale yanayopaswa kufanywa k**a wana ndoa. Mfano, kucheza pamoja, kusimulia habari za matukio fulani ktk maisha, kuongozana pamoja ktk matukio mbalimbali n.k. Si vema, wakati fulani ujisikie kwamba umeolewa na babu au umemuoa bibi. Unapaswa kumfurahia mke wa ujana wako.
4. Uwazi. Dunia sasa hivi imebadilika sana. Unapokuwa unamtafuta mwenzi wa maisha hebu jaribu kuwa muwazi kuhusu familia yako, hali yako ya maisha, kazi unayofanya, k**a una mtoto au watoto, magonjwa ya kurithi k**a yapo kwenye familia yenu n.k. Watu wengi wanadhani kwamba kumueleza mtu kuhusu kazi unayofanya kutampa shauku ya kutaka kufanya mahusiano kwa sababu ya kipato. Hivi, ni nani alie tayari ktk hali ya sasa hivi kumuoa au kuolewa na mtu ambae uwezo wake wa kujishughulisha ni mdogo? Au ni mvivu wa kufanya kazi? Kwahiyo ni vema, mkawekana wazi ili kila mmoja ajue na ajipange na namna ya kukabiliana na changamoto za familia mnapokuwa mmeamua kuwa pamoja.
5. Tabia. Peleleza vizuri ili kujua tabia za huyo unae mhitaji kuwa nae k**a mke na mme. Elimu ya mahusiano inasema kwamba gharama ya kujua tabia za mwenzi wako zisizo nzuri na kusaidiana kuzirekebisha kabla ya ndoa ni ndogo kuliko gharama ya kuzirekebisha mkiwa ndani ya ndoa. Tabia k**a ukahaba, kuvuta sigara, ulevi, uchoyo, umbea, uvivu, wizi na udokozi. Ujuapo tabia hizi kwa mwenzi wako k**a utakuwa umeamua kuwa nae kuunda familia basi msaidie kwa ushauri na kuomba pamoja ili aweze kubadilika.
6. Uandaaji wa chakula. Familia bora hustawi ktk misingi ya upendo, amani na lishe bora. Mwenzi wako hasa wa k**e ni muhimu kujiridhisha kwamba ana uwezo wa kutengeneza chakula bora kwa ajili ya mmewe na wanafamilia wengine. K**a hawezi, unaweza kumtafutia mafunzo ktk sehemu husika kwa ajili ya kuboresha uandaaji wake. Jambo hili lifanyike kwa makubaliano maalumu hasa baada ya kuridiana kwamba mtakuwa wana ndoa hapo baadae
6. Usiharakishe kufanya nae mapenzi. Tendo la ndoa linaweza kufanyika endapo wawili nyie mmekubaliana kufanya hivyo kwa lengo la kujilinda na magonjwa hasa baada ys kufahamiana vizuri historia zenu za mahudisno ya nyuma. Tendo hili lifanyike kwa umakini sana maana linaweza kuvuruga uchumba na kuacha makovu ya maumivu baada ya mmoja wenu kugundua mapungufu ya mwenzake. K**a wenzi wanaweza kuvumilana hadi safari ya kufunga ndoa inapokuwa imefika basi, tendo la ndoa lisifanyike kabisa. Barikiwa sana unapotafakari kuingia ktk edeni mpya yenye amani, furaha, upendo na kujaliana!!
Utafutaji ktk maisha haujawahi kuwa rahisi hata kidogo. Huenda mwaka unaoenda kuisha umekuwa na changamoto nyingi kiasi kwamba umeshindwa kufikia malengo uliojiwekea. Usikate tamaa.! Endelea kupambana maana huo ndio mwanzo wa kuongeza bidii zaidi na kurekebisha makosa yote uliyoyafanya 2016. Piga moyo konde na uendelee kupambana. Dharau, matusi, kukatishwa tamaa na kuachwa na marafiki ni mojawapo tu ya mambo yanayokuonesha wewe kuwa ni wa tofauti. Tambua uwezo wako kwa kila unachokifanya ili uzidi kuwa bora. Natumaini 2017 utakuwa mwaka wa mafanikio zaidi kwako. Jipange, ondoa wasiwasi, usiogope kukataliwa!!
Tumejariwa kuwa na nchi nzuri yenye utajiri wa kila namna kutokana na rasilimali zilizopo. Watanzania pia ni watu wakarimu sana na wenyenyekevu. Profesa mmoja kutoka nchi ya jirani alithubutu kusema kwamba,"watanzania ni wakarimu lakini pia ni wazembe sana, they are lazy". Huenda ni kweli. Kuna matukio mengi yanayotokea nchini mwetu yakiwa na mlengo wa kisiasa lakini yanaathiri si tu familia za walengwa lakini pia jamii nyingi za kitanzania zenye vijana wanaojaribu kupaza sauti ili kuonesha hisia zao kwamba jambo fulani haliendi sawa. Tanzania ni yetu sote wala si ya mtu mmoja mmoja. Kiongozi yeyote anapaswa kujua kwamba kuhojiwa au kukoselewa juu ya jambo fulani ndio nguzo kuu ya uongozi. K**a kweli tuna nia ya dhati ya kudumisha udugu ambao tumekuwa nao kwa muda mrefu pamoja na amani iliyodumu toka uhuru basi hatuna budi kuvumiliana na kuwa wepesi wa kusamehe. Tuijenge Tanzania kwa nguvu moja ili vizazi vijavyo vione umuhimu wa sisi tunaoishi leo. Ninayo mengi ila mimi si mwandishi mzuri. Nikipata nafasi nitayaweka kwenye maneno. Wapeni haki za kikatiba mliowak**ata, mtafuteni aliepotea akutane na familia yake na huo ndio utu.
Nakupenda Tanzania, najivunia kuwa mweusi!!
JITATHMINI
Mafanikio katika maisha ni hatua ambayo kila mmoja angependa kufikia k**a njia ya kuziishi ndoto zake.
Tuna mifano ya watu wengi sana ambao wamefanikiwa kimaisha ndani na nje ya nchi na ukisoma kuhusiana na mafanikio yao utashangaa sana maana kila mmoja huelezea jinsi alivyopambana na vikwazo vingi mpaka kufikia hapo alipo. Leo, natamani tuangalie mambo machache ambayo unatakiwa kuyatafakari na kujitathmini k**a njia ya kufikia mafanikio.
1. Tambua ndoto yako na gharama zake
Kuwa na ndoto ya mafanikio hakukufanyi wewe uwe mwenye mafanikio. Yeyote ambae unataka kufanana nae au unamwona kafanikiwa sana lazima katumia gharama. K**a unataka kuwa mcheza mpira maarufu ni lazima utambue vitu unavyohitaji kwa ajili ya mazoezi na kujiweka imara vile vile k**a unataka kuwa mjasiliamali ni lazima ukubali kujifunza namna ya kufanya shughuli za ujasiliamali, uwekezaji na nidhamu ya pesa.
2. Chagua watu wa kushirikiana nao katika kutimiza ndoto yako ya mafanikio. Mtu mmoja aitwae Jakes anasema,"If you are capable of accomplishing your dream alone then, your dream is too small" ikiwa na maana kuwa k**a unaweza kufanikisha ndoto yako mwenyewe basi ndoto yako ni ndogo sana. Katika harakati za kutimiza ndoto yako unahitaji watu wengine aidha wa kukupa ushauri na namna ya kuboresha wazo la ndoto yako au kukusapoti katika gharama zinazohitajika. Kundi hili ni muhimu sana na unapoamua kuhusisha watu wengine basi uwe muwazi na ueleze eneo ambalo unahitaji msaada.
3. Usiogope vikwazo, kukataliwa na kuanguka.
Katika kufikia mafanikio lazima ukutane na changamoto. Haijalishi ni kubwa kiasi gani. Unachotakiwa kufanya ni kutobadili focus yako. Unapokuwa unajaribu kutimiza ndoto yako kuna kukataliwa na pengine hata kudhihakiwa, usikate tamaa maana wewe ndiye ujuaye safari ulio amua kuianza. Kukataliwa sehemu moja haimanishi kwamba kila utakae jaribu kumuona atakukatalia.
4. Anza na kile ulicho nacho. Wengi wanashindwa kufikia mafanikio kwa sababu wanatamani kuanza na vitu vikubwa vikubwa. Kadiri unapoanza na mtaji mdogo katika biashara ndivyo unavyojifunza zaidi namna ya kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali katika biashara. Asilimia kubwa ya watu waliofanikiwa wameanzia chini sana na changamoto walizopitia ziliwafanya kuwa na ubunifu zaidi katika kazi zao.
5. Tambua udhaifu wako na ujitahidi kukabiliana nao. Tabia yako inaweza ikakusaidia ukatimiza ndoto yako mapema ama ukashindwa kutimiza ndoto yako. Ili ufanikiwe ni lazima uwe na nidhamu. Nidhamu ktk matumizi ya pesa( namna unavyotumia pesa yako, kuanzia wewe mwenyewe, familia na marafiki zako), nidhamu kwa watu wengine(heshimu watu wa namna zote unaokutana nao katika harakati za kutimiza ndoto yako maana hao ndiyo mtaji wako), nidhamu ktk matumizi ya muda( tumia muda wako kujielimisha zaidi katika shughuli unayoifanya ili uwe bora zaidi. Kumbuka hauko peke yako mwenye wazo hilo, wapo wengi sana. Juhudi na maarifa ndizo zitakazo kufanya uonekane kuwa bora zaidi).
6. Kuwa mtu usie ridhika. Kila siku jaribu kubuni njia mpya ya kukufanya upige hatua zaidi ktk shughuli zako. Boresha bidhaa zako au kazi yako, tafuta masoko mapya, ongezea bidhaa kulingana na mahitaji, fikiria pia kutumia teknolojia katika kuboresha na kurahisisha shughuli zako.
Kwa leo ni hayo tu. Tunawatakia wikiendi njema mnapotafakari hatua za kuchukua ili kufanikisha wazo la ndoto mlizo nazo..
Happy Valentine My X-Love
Miaka mitatu iliyopita siku k**a ya leo ulikuwa ukinikumbuka sana ukiniimbia nyimbo zilizoukonga moyo wangu japo tuliishi mbali kiasi. Nakumbuka nyimbo k**a no place that far, a woman like you, queen of my heart, you sang to me, this i promise you, i believe in you na nyingine nyingi.
Ulinipenda kwa dhati sana lkn sikujitambua na hatimae nikakusaliti kwa kufanya mapenzi na rafiki yako. Nisamehe sana mpenzi wangu. Kila wakati najutia ninapotafakari upendo uliokuwa nao kwangu. Sijapata kamwe mwanaume wa kunijali na kunipenda k**a ulivyonipenda...life has become more tough though..i wish i could be in your hands as your valentine lkn nimechelewa. Nilidanganyika kwa kukosa uvumilivu. Aliyenidanganya hanikumbuki tena. I am living in agony, i am dying for a love that i can't bring back again in place.
Happy Valentine My X-love ..because you are still the precious gold i dream for.
Msuguano wa kisiasa wa zanzibar unahitaji kuangaliwa kwa jicho la pekee sana. Kutokuwepo na maelewano ya kisiasa hupelekea kutoweka kwa hali ya amani miongoni mwa wananchi hali ambayo yaweza kupelekea ktk machafuko makubwa k**a vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Machafuko yanapotokea ni akina mama na watoto ndio wahanga wakubwa. Uchumi hudorora kwa kiasi kikubwa na pia kunakuwepo na hatari ya mlipuko wa magonjwa. Sisi sote ni watanzania, tunapaswa kukaa chini na kuzungumza pasipo kutokufikia maelewano. Ni dhamira yetu kuona tunapambana na umaskini ktk hali ya amani na utulivu.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Website
Address
P. O BOX 501
Dar Es Salaam