Unprofitable sarvants page

Unprofitable sarvants page

Share

Evangelism is our heartbeat we are dedicated to share the truth of this time in the light of the BIBLE

16/04/2024

Wengi tunatamani kubadili maisha katika nyanja mbalimbali(kiroho,kijamii na kiuchumi).MOJA YA KOSA TUNALOLIFANYA NI KUTAKA KUBADILI MAMBO MAKUBWA AU MAMBO MENGI KWA WAKATI MMOJA.Je umewahi jua kuwa mabadiliko katika maisha huanza na kubadilili MAMBO MADOGO pia MAMBO SAHIHI YANAYOWEZA KUATHIRI KWA NAMNA CHANYA MAMBO MAMBO MAKUBWA?

08/11/2018

We might not know a solution to your problem but we do know GOD who does.

Photos from Power Radio Broadcast's post 08/08/2017
12/04/2016

NGUVU YA INJILI (PART 2)
Moja ya mambo yanayochanganya wakristo wengi ni KUHESABIWA HAKI NA KUTAKASWA(JUSTIFICATION AND SANCTIFICATION)

UKWELI KUHUSU KUHESABIWA HAKI
Neno kuhesabiwa haki ni neno la.kisheria kwamba mtu Hana hatia ,(declared righteous)
1.Ulimwengu mzima umehesabiwa haki,ispokuwa haki hiyo inapaswa kupokelewa kwa hiari.Warumi 5:18-19 kila mtu duniani dhambi zake zote zimeshalipiwa.

2.Kuhesabiwa haki ni msamaha wa dhambi zote,zilizopita,za sasa na zinazokuja.MATENDO 13:38-39.SI msamaha wa dhambi zilizopita tu

3.Kuhesabiwa haki ndio kunakotufanya tuwe na amani na.Mungu si matendo yetu.Ukristo wetu mara nyingi huwa ni juu chini na mara nyingi hutufanya tukose furaha na amani.kuhesabiwa haki huleta amani na Mungu na kufanya tuwe na amani na nafsi zetu hatimaye na jirani zetu.Warumi 5:1

4.Kuhesabiwa haki peke yake ndio kunako tustahilisha kuingia mbinguni.
Warumi 5:1,Yohana 3:8,Yohana 5:24,marko :16:15,Matendo 15:1,10.Wengi huamini kuhesabiwa haki+kutakaswa ndiko kunakotuhesabia haki,lakini ni.kuhesabiwa haki kunakotustahilisha kuingia uzima wa milele na kutakaswa ni matokeao ya kustahili

5.Hatupotezi haki kila tunapotenda dhambi
NI kweli kuwa kila tunapofanya dhambi tunamuwakilisha vibaya Yesu ila si kweli kuwa tunaacha kuwa watoto wake tunapomkosea.Hata wazazi wetu wadhambi hawafanyi hivyo,kwamba usipoosha vyombo unaacha kuwa mtoto wake na sisi ni watoto kwenye familia ya Mungu Yoh 1:12.watoto hukosea na kutubu wakiwa ndani ya familia isipokuwa tu k**a wataamua kuikana famikia hiyo. God bless.
itaendelea part 3

yetu.uk

17/02/2016

The person that never makes a mistake never makes anything,and the real winner is the one who raises up from every fall and fights on. When we remember as it is our privilege to do,that CALVARY COVERS every FAULT,every FAILURE,every SIN,of the BELIEVER,then our courage is constantly renewed.

03/02/2016

NGUVU YA INJILI PART 1
Injili kwa tafsiri ya Biblia ni uweza wa Mungu uuletao wokovu kwa kila aaminiye Warumi.1:16.injili imejengwa katika kuzaliwa,kuishi,kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
Injili ni nguvu inayotukomboa kutoka katika:
1.hatia na adhabu ya dhambi (kuhesabiwa haki)
2.nguvu na utumwa wa dhambi(kutakaswa)
3.Asili ya dhambi(kutukuzwa).

Kabla ya kuelezea mambo hayo matatu,ni vizuri kuelewa tatizo la dhambi.Injili ni utatuzi wa tatizo la dhambi,mtu hawezi kufurahia utatuzi k**a hajaelewa tatizo lenyewe hasa.

Dhambi
1.Dhambi ilianza katika akili ya lusifa(shetani)Ezekiel 28:14-15
2.dhambi iliingia duniani baada ya Adam na Eva kudanganywa mwanzo 3:1-24,na kufanya shetani kuwa mungu wa dunia hii.luke 4:5-6,2kor4:4.
3.wanadamu wote waliozaliwa na adamu wamekuwa chini ya utumwa wa dhambi. 2Pet 2:9,yoh8:34,warumi 5:12,19.
4.hivyo binadamu si mdhambi kwa matendo,maneno au mawazo yake tu ba li kwa asili yake pia.zab51:5,58:3,warumi 7:14-17.
5.bila msaada wa Mungu mwanadamu hawezi tii maagizo.mema ya Mungu.warumi 8:7.
6.Mungu ni upendo,kinyume cha tabia yake ndio dhambi yenyewe yaani ubinafsi.
itaendelea sehemu ya 2

29/11/2015

Power of the gospel. coming soon.........

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


11249
Dar Es Salaam