Redfonce Mboma

Redfonce Mboma

Share

HAPA UTAJIFUNZA UFUNUO WA KRISTO YESU TU KUTOKA KATIKA MAANDIKO YA BIBLIA EVERYTHING HERE IS JESUS CHRIST

25/09/2025

LEO KATIKA KUJIFUNZA BIBLIA.

KUELEWA MITHALI HII YA YESU.

📖Mt 19:11-12 SUV
*[11] Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa. [12] Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.*

Katika Mada iliyohusu *" kuoa ,kuolewa na kuachana"* ukisoma kuanzia mstari wa kwanza ,sasa baada ya kumaliza majibu yake akachomekea mithali hiyo hapo juu kuhusu Matowashi....TUKUMBUKE KWAMBA MAFUNDISHO YAKE YOTE YALIHUSU MATESO YATAYOMPATA YEYE K**A KRISTO NA UTUKUFU UTAKAOFUATA.....

Sasa katika huo mfano wa matowashi ....NI WAHUDUMU WA NENO LA MUNGU KWA KANISA ( AMBALO NI BIBI HARUSI WA MWANA KONDOO ) k**a vile Towashi alivyokuwa MHUDUMU WA MALKIA WA MFALME...Ijapokuwa huyu Towashi ni mwanamme aliyezaliwa kuwa na sifa ya towashi au ametengwa na watu kuwa towashi au amejitoa kwa ajili ya kuwa towashi ( mhudumu wa malkia ) ijapokuwa ni mwanamme lakini asimjue malkia kwa ajili tu ya heshima ya mfalme wake.

Sasa kwa MHUDUMU WA KANISA usipojua fundisho sahihi la KRISTO, JE! UTAMLETEA MFALME WAKO BIKIRA SAFI?

👇
📖2 Kor 11:2 SUV
[2] Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.

👆
UMEONA MTUME PAULO anachosema ? Yeye ni mfano wa Towashi aliyefanywa kuwa towashi na Mungu kusudi amletee Kristo Bikira safi ( Mteule aliyefundishwa Fundisho sahihi la KRISTO)🥰🥰🥰

15/09/2025

LEO KATIKA KUJIFUNZA BIBLIA 📖

NAPENDA MTUME PAULO ANAVYOMTAMBULISHA MUNGU👇

Mungu , Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo

👇👇👐

📖Efe 1:3 SUV
[3] Atukuzwe *Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,* aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;

📖Efe 1:17 SUV
[17] *Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo,* Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;

📖Efe 3:14 SUV
[14] Kwa hiyo nampigia Baba magoti,
[ “For this cause I bow my knees unto *the Father of our Lord Jesus Christ,”*
— Ephesians 3:14 (KJV)]

📖Kol 1:3 SUV
[3] Twamshukuru *Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo,* siku zote tukiwaombea;

📖2 Kor 1:3 SUV
[3] Na ahimidiwe *Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,* Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;

📖2 Kor 11:31 SUV
[31] *Mungu, Baba wa Bwana Yesu,* aliye mtukufu hata milele, anajua ya kuwa sisemi uongo.

📖Rum 15:6 SUV
[6] ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza *Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.*

📖1 Pet 1:3 SUV
[3] Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu;

Save the Identity/ Hifadhi UTAMBULISHO

14/09/2025

14/09/2025

LEO KATIKA KUJIFUNZA BIBLIA:

UKISOMA
MWANZO 1:26-27 Kwa haraka unaweza dhania kuwa anayezungumziwa ni Adamu na hawa.

Twende pamoja

👇
*In our image*

H6754Hebrew: צֶלֶם
Transliteration: tselem
Pronunciation: tseh'-lem
----------
Description: from an unused root meaning to shade; a phantom, i.e. (figuratively) illusion, resemblance; hence, a representative figure, especially an idol; image, vain shew.

KJV usage: image (16x), vain shew (1x).

*After our likeness*

H1823Hebrew: דְּמוּת
Transliteration: dᵉmûwth
Pronunciation: dem-ooth'
----------
Description: from דָּמָה(H1819); resemblance; concretely, model, shape; adverbially, like; fashion, like (-ness, as), manner, similitude.

KJV usage: likeness (19x), similitude (2x), like (2x), manner (1x), fashion (1x).

Hapo nimekuwekea tafsiri ya maneno ya kiebrania ambayo ni *"kwa mfano wetu"* na *"kwa sura yetu"* k**a yalivyotafsiriwa biblia ya SUV.

tuyaone hayo maneno katika lugha ya KIYUNANI

👇
Kol 1:15 ; 2Kor 4:4; Rom 8:29( man in christ );1kor 11:7(man in christ );1kor 15:49 (both); 2kor 3:18 ;kol 3:10( man in christ)

G1504Greek: εἰκών
Transliteration: eikṓn
Pronunciation: i-kone'
----------
Description: from εἴκω(G1503); a likeness, i.e. (literally) statue, profile, or (figuratively) representation, resemblance:
Translation: image.

KJV usage: image (23x).

Hapa neno liko moja *"Eikon"* lenye maana rahisi 👉 *WASIFU* au *PROFILE*

ILI KUPATA USAHIHI WA MENENO KATIKA BIBLIA LAZIMA TUSOME YOTE ,KWA SABABU HAKUNA NENO LENYE MAANA MOJA KATIKA BIBLIA NZIMA.

Maana ya Neno tutaipata tukisoma katika mkitadha wake.

Kwa sababu maandiko ya agano la kale (Mwanzo hadi Malaki) yaliandikwa kuhusu Kristo atakayekuja....

👇
📖Luka 24:25, 27 SRUV
[25] Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!
[27] Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.

soma pia mstari wa 44-46.

📖Yohana 5:46 SRUV
[46] Kwa maana k**a mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.

So MUSA ALIANDIKA HABARI ZA KRISTO kuanzia kitabu cha Mwanzo...

KATIKA KITABU CHA MWANZO UZAO WOTE WA ADAMU haukuchukua SURA YA MUNGU bali SURA YA ADAMU👇

📖Mwanzo 5:3 SRUV
[3] Adamu akaishi miaka mia moja na thelathini, akazaa mwana *kwa sura yake, kwa mfano wake,* akamwita jina lake Sethi.

Mtume Paulo akiwa mwandishi wa ufunuo wa Kristo ( kufunua maandiko ya agano la kale) anasema ,WALIOMWAMINI KRISTO WAMEPEWA AU WAMEZALIWA KATIKA SURA YA KUFANANA NAYE AU SURA YA MBINGUNI.

waliozaliwa na Adamu wamechukua sura ya Adamu, na waliozaliwa katika Kristo wamechukua sura ya kristo.
👇

📖1 Wakorintho 15:49 SRUV
[49] Na k**a tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.

[ kuna sura ya udongo/ adamu na sura ya mbinguni/ Kristo]

📖📖Warumi 8:29 SRUV
[29] Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

[ “For whom he did foreknow, he also did predestinate to be conformed to the image of his Son, that he might be the firstborn among many brethren.”
— Romans 8:29 (KJV)]

📖2 Wakorintho 3:18 SRUV
[18] Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, k**a vile katika kioo, *tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, k**a vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.*[“For whom he did foreknow, he also did predestinate to be conformed to the image of his Son, that he might be the firstborn among many brethren.”
— Romans 8:29 (KJV)]

So maandiko yanatuthibitishia kwamba KRISTO Yesu ndiye sura / wasifu / mwonekano halisi wa Mungu na siyo Adamu.

09/09/2025

sehemu ya 3.

CHORA MSTARI / UWE MHUDUMU WA AGANO JIPYA.

*AINA ZA SADAKA HUAKISI AINA YA AGANO ULITIMIKIALO:*

📖1 Kor 9:13-14 SUV
[13] Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? [14] Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.

Katika Agano la kale kwa maagizo ya Musa kuna uzao wa Lawi walioteuliwa kupokea sadaka , na waligawanywa katika makundi mawili ambayo ni:
1. wahudumia madhabahu ; Haruni na uzao wake tu.
2. wahudumia hema ya kukutania ; walawi ambao waligawanywa kwa makundi matatu ambao ni :
(a) Wagershomu
(b) Wamerari
(c) Wakohathi
Hawa walichaguliwa watumike badala ya wazaliwa wa kwanza.( Hes 3:12...).

👇👇
Soma vizuri hii mistari;

📖1 Kor 9:13-14 SUV
[13] Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? [14] Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.

Mtume Paul amefunua maandiko ya Musa kwamba ,Wahudumu wa madhabahu ( Makuhani wa uzao wa Haruni posho yao ilitokana na kilichotolewa juu ya madhabahu. Ni kitu gani kilichotolewa juu ya madhabahu? Jibu ni sadaka ya KUINULIWA au kwa jina lingine inaitwa ZAKA YA ZAKA...Soma Hes 18:....).
Mtume Paul anaendelea kufunua kwamba Wahudumiao hema ya kukutania ( ambao ni walawi katika jamaa ya Gershomu,Merari na kohathi.Hao posho yao ni sadaka zitolewazo katika hema ya kukutania ambazo ni zaka ( fungu la kumi aina ya kwanza.kwa sababu kuna aina tatu katika maagizo ya Musa).Soma zaidi Hes 18.
Hizi aina mbili za watumishi au wahudumu na sadaka walizopokea zinaakisi uhudumu kwa AGANO LA KALE.

Aina ya tatu ya huduma na sadaka ambayo Mtume Paulo amefunua ni huduma ya kuhubiri Injili na sadaka yake yake kwa ajili ya posho ya hao wahubirio injili.Hii ndiyo huduma pekee kwa AGANO JIPYA.

AGANO JIPYA halina huduma ya kuhani wa kuhudumia madhabahu ( ambayo nayo haipo katika agano jipya) ,wala haina huduma ya hema kwa sababu hatuna Lawi wa kuhudumia hema ( ambayo haipo ).Madhabahu ilikoma na sheria yake ,na hema ya kidunia ilikoma na sheria zake.Sasa tunayo hema Mpya ambayo mhudumu wake anakaa ndani yake yaani Kristo Yesu ndani Yetu.

ZAKA ili iwe Zaka kimaandiko ni lazima iwe na sifa zifuatazo;

1. iwe ni sehemu ya 10
2. iwe nisehemu ya mazao ya shamba
3. tatu k**a ni fedha ni lazima ibadilishwe kuwa thamani katika madhao,maana yake ile fedha inunue mazao ndiyo yatolewe
4. mpokeaji ni lawi kwa sababu yeye alitoa akiwa viunoni mwa Ibrahimu alipokutana na Melkizedeki
5. Apokeaye haruhusiwi kuwa na urithi wa ardhi katika nchi yake ( kanaani ) kwa sababu ile 10% apokeayo ndiyo urithi wake kutoka kwa Bwana.
6. lawi peke yake ndiye atahudumia hema na kuchukua uovu wa watoao zaka na hao watoao zaka hawaruhusiwi kukaribia hema na wakifanya hivyo watakufa.

itaendelea...

01/09/2025

CHORA MSTARI/UWE MHUDUMU WA AGANO JIPYA

Tunaendelea na sehemu ya 03.

Katika somo lililopipa tuliangalia vile watu wa zamani walivyohesabiwa haki kwa imani ya yule atakayekuja,ijapokuwa matendo yao mengi yalikuwa mabaya...nikatolea mfano akina mfalme Daudi alivyoua ,au Samsoni nk.

Sasa tuangalie upande mwingine...UWEPO WA AGANO LA KALE KATIKA VITABU VYA AGANO JIPYA....

Rum 10:1-4 SUV
[1] Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe. [2] Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. [3] Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. [4] Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.

Wayahudi ambao hawakuamini ufufuo wa KRISTO na wakataka kuhesabiwa haki itokayo kwa Mungu kwa njia ya matendo yao ,HAWAKUIPATA...Mtume Paulo anasema " wanajuhudi kwa ajili ya Mungu ,lakini si katika maarifa.."

tunaweza kusema hivi ,hawataki maarifa ya Mungu ...yaani Ufunuo wa ile kweli ( Revelation knowledge) tuliyoipokea kwa njia ya Roho wa Mungu.Wanataka maarifa ya kihisia yanayopatikana kwa njia ya milango mitano ya fahamu ( sense knowledge ) ili kuwapa ufahari.

Mambo ambayo kanisa la kwanza liliyashika kipindi cha mpito( transition era ) ,kipindi cha kutoka kuhama kimaarifa kutoka mwilini ( hisia ) kuja rohoni ( ufunuo) ambayo yalikuwa ya sheria ya Musa na mapokeo kutoka kwa mababa kwa mfano...kutawadha, ukabila (uyahudi/ judaism ), sheria za vyakula ,sikukuu za kuandama mwezi nk Hayo yote yalileta mkanganyiko kwa kanisa la kwanza hadi zamani za Ujio wa mtume Paul.

itaendelea..

24/08/2025

tuendelee kidogo. NO.2.

CHORA MSTARI / UWE MHUDUMU WA AGANO JIPYA.

📖2 Kor 3:6 SUV
[6] Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.

UWEPO WA AGANO JIPYA KATIKA MAANDIKO YA AGANO LA KALE.

Hapa nimechukua mkitadha wa mpangilio wa vitabu vya agano la kale ambapo kitabu cha Mwanzo kimejumishwa kuwa ni sehemu ya maandiko ya agano la kale ijapokuwa si sehemu ya agano lile.

Agano jipya katika maandiko ya agano la kale limetokea katika AHADI, yes Ahadi ya kweli kwa sababu walioamini Ahadi ile hawakupotea ijapokuwa ilikuwa ya kusubiria / taraja, k**a tuonavyo mwandishi wa kitabu cha Waebrania 11 anavyoelezea Imani yao watu wa kale kabla ya Msalaba.

👇
📖Ebr 11:1-2, 13, 39-40 SUV
[1] Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. [2] kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa.
[13] Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.
[39] Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; [40] kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.

Tukisoma katika kitabu cha Mwanzo

📖Mwa 3:15 SUV
[15] nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.

Ahadi ya mzao tunaipokea kwa kuamini kazi ya msalaba na si kwa kufanya kazi maana k**a ingekuwa kwa jitihada zetu isingelikuwa kwa neema bali k**a ujira.

📖Mwa 15:6 SUV
[6] Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.

Ibarahimu aliamini tu naye Mungu akamhesabia haki.Haki kwa njia ya Imani tu na siyo kwa njia ya matendo.

Ibarahimu aliamini nini?
Jibu ni : Aliamini Ujio wa Kristo atakayekuja ( Kufa ,kuzikwa na kufufuka ).
👇
📖Rum 4:13, 17-22, 24-25 SUV
[13] Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa imani.
[17] (k**a ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako. [18] Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, k**a ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. [19] Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa k**a miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara. [20] Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; [21] huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. [22] Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.
[24] bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu; [25] ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.

Hebu Angalia wana wa Israel waliosafiri na Musa jangwani ijapokuwa walitumukia Agano la adhabu/ dhambi/ la mauti lakini Mungu hakuwaacha bila kuwaonesha Agano jipya katika ahadi wapate kuheaabiwa haki ipatikanayo kwa imani....

📖Hes 21:8-9 SUV
[8] Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. [9] Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

👆walioumwa na nyoka hawakuishi kwa sababu ya kutazama nyoka wa shaba bali kwa sababu waliamini...

Yesu amesawazisha kwa ufafanuzi ufuatao:

👇
📖Yn 3:14-15 SUV
[14] Na k**a vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; [15] ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.

ishu siyo waliomtazama Kristo alipoinuliwa au alipotundikwa juu ya mti bali walioamini kwamba kifo chake kilikuwa ni sadaka kwa ajili ya ondoleo la dhambi hao ndiyo wapokeao uzima wa milele ,iwe ni wa wakati wa Musa ( imani ya tarajio ) kwa wakati wetu ( imani timilifu kwa sababu aaminiye anapokea ahadi wakati ule ule anaposikia na kuamini ).

Ukisoma maandiko ya agano la kale utaona kuna wateule wengi sana ambao walitenda mambo mabaya kwa mfano Samsoni aliua watu wengi sana ,Mfalme Daudi aliua watu wengi sana ,nk Lakini kwa sababu ya ile imani ya mzao wa Ibrahimu walihesabiwa haki.

Itaendelea..

09/08/2025

LUCIFER NI JINA LA MSIMBO ( CODE NAME ) LA MFALME NEBUKADNEZZAR WA BABEL.

Ijapokuwa Kazi za Stephen langton na Robert Estienne ) karne ya 13 na 16 baada ya Kristo ) za kugawa Biblia katika sura na Mistari tunayoiona imesaidia watu wengi kusoma Bibilia na kufanya marejeo lakini imechangia kwa sehemu kubwa kuwafanya hao wasomaji wasielewe kwa urahisi maandiko yake kwa sababu walivuruga pakubwa mipangilio ya mkitadha wa waandishi wake.

Embu fikiria leo wasomaji wangapi wanaamini LUCIFER KUWA NI ROHO ilihali ukisoma katika mkitadha wake jina linaonekana kuwa ni jina la siri ( code name ) kwa Mfalme Nebukadnezzar?

Neno la kiebrania lililofasiriwa kwa kilatini kiwa ni lucifer na linapatikana mara moja tu kwa Biblia ya kiebrania ( Tanakh )
👇👇
H1966Hebrew: הֵילֵל
Transliteration: hêylêl
Pronunciation: hay-lale'
----------
Description: from הָלַל(H1984) (in the sense of brightness); the morning-star; lucifer.

KJV usage: Lucifer (1x).

👆👆
Mkitadha wake unaanzia kitabu cha Isaya sura ya 13:1- 14:32

Ukiwa na muda wa kutosha soma huo mkitadha na Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo akupe roho ya hekima na ya ufunuo kuelewa Unabii wake.

28/10/2024



UBATIZO MMOJA NI UPI?

Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja,
Waefeso 4:5

Kanisa lilipozaliwa lilihitaji sana kuelewa fundisho la Kristo , hivyo iliwachukua miaka kadhaa kuyaacha mapokeo ya mababa na vivuli vilivyotumiwa na manabii kumwelezea Kristo atakaye kuja.

Soma zaidi👇👇

Yohana Mbatizaji alikuja akibatiza kwa maji... na UJUMBE WAKE ulikuwa huu

📖Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
Mathayo 3:11

au

📖Naye alihubiri akisema, “Baada yangu atakuja yeye aliye na uwezo kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”
Marko 1:7-8

au

📖Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji. Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. ”
Luka 3:16

UKIELEWA HAPO JUU katika hivyo vifungu vya waandishi watatu utaona Yohana aliweka wazi kabisa ... kwamba YEYE NDIYE ANABATIZA KWA MAJI kwa ajili ya kumtambulisha atakaye kuja baada yake. Jana niliuliza swali ... kwa nini Yesu anasema Yohana Mbatizaji ndiye mkuu kuliko watu wote waliozaliwa na Mwanamke?

Jibu lake ni hili hapa:👇
Manabii wote waliotangulia kabla yake walitabiri wakisema ... "Bwana Mungu asema" au " Hivi ndivyo asemavyo Bwana..." .... Lakini kwa Yohana Mbatizaji ilikuwa tofauti , Yeye huduma yake ilikuwa ... " Huyu ndiye ...." Hivyo Ukuu katika Ufalme unaelezewa kulingana na kiwango cha UFUNUO wa kumjua Kristo na siyo kiwango cha kufanya miujiza.

Niendelee na somo la Ubatizo....

Tumeona Jinsi Yohana Mbatizaji alivyotangaza... kwamba ajaye baada yake ATABATIZA KWA ROHO na siyo kwa maji.

Lakini baada ya Kristo kuondoka ( kuondoka kwake ndiyo ilikuwa kuingia ndani yao)... Kanisa la mitume liliendeleza ubatizo wa Yohana wa kuwazamisha watu kwa maji... kwa nini ? kwa sababu wao nao walikuwa hawajajua kwa usahihi Fundisho la Kristo .

UJIO WA MTUME PAULO ULILETA UKAMILISHO WA FUNDISHO LA KRISTO.

Mafundisho ya Mtume Paulo ni Ufunuo wa Kristo ambao si wa ushuhuda wa macho ( eye witness account / sense knowledge ) na hii ni kwa sababu hakufundishwa na Mitume walioishi na Kristo wakati wa huduma yake. K**a alivyoandika hapa👇

📖Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu. Kwa maana mimi sikuipokea hiyo Injili kutoka kwa mwanadamu, wala sikufundishwa na mtu, bali niliipata kwa ufunuo kutoka kwa Yesu Kristo.
Wagalatia 1:11-12

📖Lakini ilipompendeza Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu na kuniita kwa neema yake, alimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu wa Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu yeyote, wala sikupanda kwenda Yerusalemu kuwaona hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda mara moja Arabuni na kisha nikarudi Dameski.
Wagalatia 1:15-17

KATIKA HUDUMA YAKE YA INJILI MTUME PAULO AKAFIKA EFESO...

Huko Efeso akawakuta wanafunzi waliokuwa wamebatizwa UBATIZO WA YOHANA yaani wa kuzamishwa katika maji...

📖Apolo alipokuwa huko Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso. Huko akawakuta wanafunzi kadhaa, akawauliza, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?”
Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.” Ndipo Paulo akawauliza, “Je, mlibatizwa kwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Kwa ubatizo wa Yohana.”
Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohana ulikuwa wa toba, aliwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja baada yake, yaani, Yesu.” Waliposikia haya, wakabatizwa katika jina la Bwana Yesu. Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia, nao wakanena kwa lugha mpya na kutabiri. Walikuwa k**a wanaume kumi na wawili.
Matendo 19:1-7

Sasa hapa ndipo Madhehebu yalipochanganywa yakachanganyikiwa.

FUNDISHO POTOFU LINATIKANA NA SABABU MOJAWAPO AU ZOTE KATI YA HIZI ZIFUATAZO;

1. kupindisha Kweli
2. kuongezea kitu katika ile Kweli
3. kuondoa kitu katika ile Kweli

NB: neno "Kweli" hapo linamaanisha "Mtu ambaye ni Kristo" na hapa ninazungumzia fundisho la Kristo ( Mtu ).

Sasa Madhehebu mengi yameacha ubatizo wa Roho ambao ndiyo Paulo aliwasahihisha wale watu wa Efeso ... na ambao pia tumeona Yohana Mbatizaji alisema yeye ajaye baada yake ATABATIZA KWA ROHO....

soma hii itakisaidia

📖Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini sababu ya kuja nikibatiza kwa maji ni ili yeye apate kufunuliwa kwa Israeli.”
Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni k**a hua, akakaa juu yake. Mimi nisingemtambua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia na kukaa juu yake, *huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’* Mimi mwenyewe nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.
Yohana 1:31-34.

YESU NAYE AMEFUNDISHA KUHUSU UBATIZO:

📖Wakati mmoja alipokuwa pamoja nao, aliwapa amri hii, “Msitoke Yerusalemu, bali ingojeni ahadi ya Baba, ambayo mmenisikia nikisema habari zake. Yohana aliwabatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
Matendo 1:4-5

Ubatizo mmoja ambao Mtume Paulo anafundisha ni ule wa Roho yaani Mungu kukaa ndani ya mwamini na siyo mwamini kizamishwa ndani ya maji.

Kanisa kuacha fundisho la Ubatizo wa Roho ambao abatizaye ni Kristo na wahudumu wa Injili kujivuka UYOHANA MBATIZAJI kumepoteza nguvu halisia za Madhihirisho ya Roho wa Mungu kwa makusanyiko.

Imeandaliwa na ...

Bible comentary ( Sir Redfonce Mboma ).

October 26,2024 19:30-20:30.

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
18:00 - 19:00
Sunday 12:00 - 20:00