Keys Educational and Stationery Services - KESS

Keys Educational and Stationery Services - KESS

Share

For the best and quality educational & stationery services

27/10/2024

Now available for Tsh.15,000 . Free delivery. Contact: 0758587618/0679587618

30/11/2023

You're welcome

17/04/2023

Baada ya kupitia CHANGAMOTO nyingi katika kuelekea ndoto yake ya kuwasaidia wananchi wenzake wa Afrika Kusini,

Baada ya kukutana na VIKWAZO vikubwa kuelekea SHAUKU yake ya kuwa RAIS wa NCHI yake,

Baada ya kufungwa kwa Miaka 27 na kila mtu akidhania kuwa amefika mwisho,

Nelson MANDELA akafanikiwa kuwa Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini.

Ndipo aliposema “The greatest GLORY in living lies not in NEVER FAILING, but in RISING everytime we FAIL”

Akimaanisha, utukufu mkubwa(Mafanikio makubwa) kwenye maisha, hayatokani na wewe KUTOKUSHINDWA bali hutokea pale ambapo UNAINUKA kila wakati BAADA YA KUFELI.

Chochote ambacho kinaonekana KIMEKUSHUSHA CHINI, tukio lolote ambalo linaonekana UMEFELI,

Usisahau kuwa huo ni MTAJI wa KUKUPA ushindi MKUBWA mbele yako. Amua kuinuka, kujipanga tena na KUSONGA mbele.

Usisahau hili, “It’s not over, until it’s over”. Haijaisha hadi imefika mwisho.

Ukimaliza Kuisoma, nisaidie kuishare tafadhali.

See You At The Top



05/10/2022
01/08/2022

KESS PLATFORM wishes all the best Standard Seven Pupils in Dar es salaam region in their Regional Examination that commences today.

09/01/2022

Now available for only 15,000/= Tsh

27/10/2021

*KILA LA HERI DARASA LA NNE 2021*

*Keys Educational and Stationery Services (KESS)* tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa shule na taasisi mbalimbali za kielimu ambazo zimekuwa nasi katika mwaka wa masomo 2021.

Ikiwa yamebakia takribani masaa kadhaa kwa watoto wetu wa darasa la nne waanze upimaji wao wa kitaifa, tunajivunia kuwa sehemu ya maandalizi ya watoto hao.

Mwaka huu tumehudumia maelfu ya wanafunzi kupitia vitabu vyetu vya mazoezi pamoja na mitihani mbalimbali.

Tunao ujasiri na matumaini makubwa kwamba wanafunzi wetu wa darasa la nne watafanya vizuri katika upimaji wa kitaifa unaotarajiwa kuanza kesho.

Aidha, tunawakumbusha wadau wetu kuwa mwisho wa maandalizi ya darasa la nne wa mwaka huu ni mwanzo wa maandalizi ya darasa la nne wengine wa mwaka 2022.

Tunawaalika tena kufurahia huduma zetu kwa mwaka mwingine wa masomo 2022. Tayari tumeshatoa kalenda yetu ya mwaka ujao ili kwa wale ambao hawakubahatika kujiunga nasi mwaka huu waweze kupanga bajeti zao za za mwaka ujao.

Kwa Sasa nguvu tunaielekeza kwa madarasa yanayobaki ikiwemo darasa la tatu,tano na sita.

Tayari tumeshaandaa series za mitihani kwa madarasa tajwa hapo juu kwa ajili ya kuwapika wanafunzi wetu.

Mitihani yetu imekuwa msaada mkubwa kwani siku zote tumekuwa tukizingatia ubora na viwango vinavyotakiwa.

Karibuni kwenye mtihani wetu wa darasa la sita utakaofanyika tarehe 4 & 5 Novemba 2021.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu huduma zetu usisite kutupigia simu namba 065836694 au 0758587618.

Waweza pia kutembelea ofisi zetu zilizopo mtaa wa Kifuru, Barabara ya Kinyerezi-Mbezi.

🙏Mungu awabariki!

Photos from Keys Educational and Stationery Services - KESS's post 29/05/2021

Mkurugenzi wa KESS Mwalimu Gozbeth Leonard Baruti akikambidhi cheti na zawadi mwanafunzi Aymar Mohammed wa Shule ya Msingi na Msingi Rainbow King'azi aliyeshika nafasi ya kwanza katika mtihani wa kwanza wa utamilifu wa KESS ulofanyika mwezi Aprili 2021

01/05/2021

Hatimaye Salome Andrew na Elias Lukata wa Bright Star Kigoma ambao walikuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora katika mtihani wetu wa darasa la saba uliofanyika mwezi machi,wapokea vyeti vyao vya pongezi kutoka KESS.

Wiki ijayo tutawatembelea wanafunzi kumi bora katika mtihani wa darasa la nne.

Aidha tumeamua kuboresha zawadi zetu kwa mshindi wa kwanza, wa pili na watatu, ambao licha ya kuwapatia vyeti, tumewaandalia pia na zawadi nyingine nzuri.

Malengo yetu ni kuamsha ari ya kujisomea miongoni mwa wanafunzi na kuwaambukiza shauku ya kuwa washindani.

KARIBUNI KWA MTIHANI MWINGINE WA DARASA LA SABA MEI 20 & 21, 2021.

*WE UNLOCK THE DOORS OF SUCCESS*

Photos from Keys Educational and Stationery Services - KESS's post 15/12/2020
17/05/2020

Coming soon .......

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00