30/10/2021
K**a unataka kujifunza kuhusu hisa, kupata vitabu kuhusu hisa , kujua namna ya kuwekeza katika kampuni kubwa duniani k**a TESLA GOOGLE AMAZONE NA KAMPUNI NYINGINE NYINGI unakaribishwa telegram groups kwa ajili ya kujifunza pamoja fata link 👇👇
UWEKEZAJI WA HISA
STOCK LEARNING COMPANY ANALYSIS STOCK SIGNAl
23/10/2021
HISA V/S HATI FUNGANI.
hisa na hati fungani ni miongoni mwa bidhaa zinazopatikana katika msoko ya kifedha.
tofauti iliyopo kati ya hisa na hati fungani ni k**a ifuatavyo,
HISA ni umiliki wa sehemu ya kampuni mfano; kampuni yako inashida ya kifedha unabidi umshawishi mtu aweke fedha katika kampuni yako ili awe sehemu ya umiliki hapo anakuwa mwanahisa.
lakini hati fungani ni mkopo unaoombwa na kampuni kwa makubaliano ya ongezeko fulani kwa muda maalumu mfano; kampuni yako inashida na fedha unakuja kukopa kwangu kwa makubliano ya kuirudisha kwa ongezeko la faida fulani mfano onezeko la asilia 10 mpaka 15 kwa kiwango ulichotoa.
tukutane kesho kwa tofauti nyingine za HISA na HATI FUNGANI, asante.
mwl Aidan Mponeza
07/01/2021
MAANA YA HISA HATIFUNGANI NA TOFAUTI ZAKE:
HISA:
👉Ni sehemu ya umiliki wa kampuni flani mfano:; wewe una kampuni lakini umepeleza pesa unaingia kwenye SOKO la hisa kukutana na wekezaji wenye pesa.
MWANAHISA NI NANI.?
👉Ni mtu anayemiliki hisa za kampuni flani kupitia soko la hisa.
UNAZIPATAJE HIZO HISA.?
👉 Katika SOKO la hisa mfano Tanzania Ni soko la hisa la dar es salaam.
KIWANGO CHA KUNUNUA HISA.?
👉Gharama zinatofautiana kulingana na kampuni mfano crdb leo hisa yao moja wanauza 195 Tsh/= na KIWANGO ya kununua HISA kimo Cha chini Ni hisa 100 kwahiyo kwa ghara ya 19500 inatosha kupata hisa crdb.
Ok leo tuishie hapa K**a Kuna swali utauliza tuje kwenye HATI FUNGANI.
HATI FUNGANI.
👉mkopo unaoombwa na kampuni au serikali kwa makubaliano maalumu kwa muda maalumu.
✔️mfano bajeti ya serikali ya fedha inapopelea kwenye baadhi ya wizara serikali inaamua kutoa HATIFUNGANI kwa wananchi watakaoweza kununua ili yenyewe kupata fedha.
MMILIKI WA HATIFUNGANI.
👉Mmiliki wa hatifungani Ni mkopeshaji wa kampuni au serikali, yeye huyu hajui Kuna kupata hasara Bali yeye anachojua Ni faida TU.
NAMNA YA KUNUNUA HATIFUNGANI.?
👉Hatifungani unamiliki mtu yeyote mwenye zaidi ya umri wa miaka 18 na utakubaliana na makubariano husika.
✔️mfano NMB walikuwa wanauza Hatifungani zao 2019 kwa ghara zinazoanzia laki 5, kwa ongezeka la faida ya 13% kila mwaka kwa muda wa miaka 3.
Kwa leo niishie hapo ndugu MUNGU akubariki kesho nitaendelea nisikuchoshe sana nakutakia siku njema.
©Mwl: Mponeza
02/01/2021
PASSIVE INCOME (KIPATO KISICHO MOJA KWA MOJA):
✓hii Ni aina ya kipato ambacho hakikuitaji moja kwa moja katika utengenezaji wa faida yaan kinachoitajika toka kwako Ni pesa(ushasikia pesa ikufanyie kazi Basi ndio hi passive income hii)
Unajua tunaishi katika kizazi Cha ajabu Sana ambacho unaweza kuuza suti ofisin ikiwa wewe upo uchi kitandani umelala. Ukimbisha mcheki mrakilikubwa
Yaani namaanisha kwamba kwa teknolojia tuliyofikia unaweza kuwa sehemu ya umiliki wa kampuni fulani huko ughaibuni ilhali wewe upo hapo, ilemela MWANZA au hata mwanga kigoma. Wala sio ajabu mmmmh Kuna watu nafsi zimeanza kusema Aidan porojo. Just wait.. tunaenda mdogo mdogo utanielewa TU Mimi ndio mwl: Mponeza.
Kwa wepesi huu wa teknolojia Basi tunapata nafasi ya kuwekeza katika sehemu mbalimbali hasa katika masoko ya bidhaa mitaji na fedha ndani na nje ya mipaka ya tanzania🙊🙊 kwa kuwekeza katika HISA, HATIFUNGANI pamoja na BIDHAA k**a cocoa, sukari, dhahabu, pamba,silver na zingine nyingi.
Kwanini uingie kwenye aina hi ya uwekezaji utakao kuletea kipato Ni kwamba Ni rahisi Sana kuiongoza hatar ya kupata, pili inakurahisishia muda, tatu inaweza kuwa urithi kwa kizazi chako.
Ok kwa leo tunaishi hapo kipindi kinaachofuata Ni kuhusu maana ya
HISA NA HATI FUNGANI PIA TOFAUTI ZAKE tuonane kesho hiyo uwe na siku njema.
©Mwl: Mponeza
30/12/2020
Mwl:Mponeza.
Rafiki yangu huu mwaka nitatoa kile nilichonacho kwa mtu ambae Hana.
Sina fedha au Mali ya kukupa ila nitakacho kupa huu mwaka Ni zaidi ya fedha Ni zaidi ya mali.
Kwa wanaonufahamu kidogo TU watashuhudia ya kuwa Sina tabia ya kufunika vitabu nilivyosoma.
Huu mwaka nakwenda kukupa bonge moja la nondo nakwenda kukupa maarifa ya kutosha jitahidi kuwa TU Aidan karibu.
Yaani mpaka inafika 2021 muda K**a huu utakuwa mtaalamu wa masoko ya kifedha hasa kwenye.
1.HISA(stocks)
2.bonds (hati fungani).
3.commodities.(bidhaa)
Yaani utawezaje kuwa sehemu ya umiliki wa kampuni K**a.
1.CRDB
2.NMB
3.JATU
4.KENYA AIRWAYS..
5.APPLE
6.GOOGLE
7.TESLA
8.facebook.
Yaani umezoea serikali inakukopesha wewe Sasa nitakupa maarifa ya kuikopesha serikali na Kisha ikulipe faida 🤣🤣🤣🤣 Ni very simple kuwa nami karibu.
K**a tutakuwa pamoja this year dondosha comments chini Ni kheri ukawa na maarifa halafu usiyafanyie kazi kuliko kuyakosa kabisa.
3.com
22/12/2020
Ngoja nimalizie wino wangu✍️✍️✍️✍️
ITAKUCHUKUA MUDA.🤔🤔
🔹unajua itakuchukua muda kupata unachokitaka.
🔹Kiukweli jinsi muda unavyokimbia unaweza tamani ushikilie mshare wa saa uigandishe dunia kidogo ili ukamilishe mambo yako kidogo then uachie twende sambamba.
🔹But MUNGU aliliona Hilo akaona aiondoe hiyo nafasi ili Kila mtu akimbie mbio zake.
🔹For sure🤔🤔 unatamani kufika pale unapotaka but inabidi ukubar ya kuwa inakuhitaji kulipa gharama.
🔹Gharama ya muda inaambatana na uvumilivu, maumivu yauvumilivu hupunguzwa na ufanisi na jitihada.
🔹Kwahiyo usitupe dira baharini kwa uchovu wa urefu wa safar NO endelea kujipa muda usichoke.
🔹Ukiacha sasa UMESHINDWA ukiendelea UTASHINDA usipoteze mwelekeo.
22/12/2020
Habari.!
Ndugu zangu wa fikialengo now am back nikiwa na energy kubwa Sana masomo tutakayo kwenda nayo this year Ni ya Moto Sana.
1.nguvu ya falsafa,
2.kipato kisicho Cha moja kwa moja.
3.nguvu ya MAARIFA.
Tumuombe MUNGU uzima.
26/04/2020
Nussery SEBURENI KWAKO
NUSSERY SEBURENI KWAKO:
Kwa wazazi wenzangu pamoja na kuwa na wakati huu mgumu wa kipindi cha Corona lakini elimu kwa mtoto haikomi.
Tunavyo vitabu vya watoto wa kuanzia miaka 2-6 vitakavyo mfanya kuwa busy na kuwa na kumbukumbu na shule na kupata maarifa akiwa nyumban.
Mwalimu unaweza kuwa wewe mzazi au vijana wako walio nyumbani na mtoto akaelewa.
VITABU tulivyonavyo.
1. Kujifunza namba kwa lugha ya kiingereza.
2. Kujifunza kusoma herufi kwa kiingereza.
3. Kujifunza kuchora picha za wanyama na mimea.
4. Kujifunza majina ya vitu mbalimbali kwa kiingereza.
5. Kitabu vya michezo ya kuchangamsha ubongo.
NB: Vitabu vinapatikana kwa gharama ya 2000Tsh
WhatsApp number 0685042529
08/01/2019
FURSA.
kuna muda unaletewa fursa ndo unaisikia kwa mara ya kwanza lakini ukaamua kuidharau kwamba haikufai.
Baada ya muda kupita unasikia ile fursa uliyofikishiwa imenufaisha watu kwa mazingira yaleyale.
Kumbe kipindi unafikishiwa uliitajika kuifahamu kwa undani zaidi ili kipindi unaamua kutokuifanya basi unaamua kwa vigezo na sababu maalumu sio kwa dharau zako.
Hii itakusaidia kufahamu fursa za namna hiyo nakukusaidia kuokoa muda siku ukiletewa kwa mara ya pili.
©Aidan mponeza.
Mwandishi/
Mshairi/
Mshauri/
Mhamasishaji/
03/01/2019
PAKA BAUNSA.
katika ulimwengu wa wanyama kuna vijiji viwili tofauti vilivyo kuwa jirani sana walikuwa wakiishi paka na panya, paka kijiji. A na panya Kijiji B.
Siku moja paka baunsa alikwenda kutembea kwenye kijiji walichokua wanaishi panya, ghafla panya walivyomuona wakaanza kukimbia kwa lengo la kuokoa maisha yao.
k**a unavyojua ndugu yangu bifu kati ya panya na paka, lakini katika kundi la panya waliokuwa wanakimbia paka BAUNSA alimuona panya mmoja akikimbia kwa shida sana na alilalama kwa maumivu sana.
Paka baunsa moja kwa moja alitambua maradhi aliyokuwa akiuguria yule panya akamwonea huruma na kuanza kukimbiza kwa kasi zaidi ili amsaidie.
Lakini yule panya akaanza kuhofia ile kasi ya yule paka na kwanini umuandame yeye akaamua kumsubiri ili akabiliane naye.
Lakini paka bausha alivyomfikia akamk**ata yule panya kisha kumueleza kuwa yupo kwa ajiri ya msaada na sio kumuangamiza.
Na baada ya kumsaidia wakawa marafiki tukutane tena kesho kuna cha kukupa kingine kuhusiana na paka BAUNSA na panya.
......SOMO LA KUJIFUNZA.....
=>kuna muda maisha ya wengine ni bora sana kuliko njaa zako.
=>Adui yako pia anahitaji kusikilizwa mpe muda.
=>kuna muda utaandamwa na shida, changamoto, umasikini lakini hatima yako sio ya kutabiri kwa mtazamo hasi.
=>changamoto mpya zipo kwa ajiri ya kukuletea watu wapya zichunguze vizuri.
©aidan mponeza.
instaAidan Mponeza
23/12/2018
SILAHA YA 03.. 2018/2019.
ndani ya mwaka 20172018 katika harakati zangu za kupata maarifa niliweza kufanikiwa kukutana na kazi za waandishi wengi tu ndani na nje ya Tanzania.
mfano:makirita amani, joel nanauka, erick shigongo, tonny robins, brian tracy, robert kiyosaki, Shaban robert, napolean hill, na wengine ambao sijawaorodhesha.
Ndani ya vitabu vya hawa waandishi kulikuwa na mada mbalimbali walizofundisha lakini cha ajabu waandishi karibia wote kwenye uandishi wao kuhusu mafanikio walisisitiza sana kuhusu kujiwekea malengo.
mwishoni mwa mwaka 2017 k**a ilivyo sasa hivi mwezi wa 12 nilikutana na work book ambayo imeandaliwa na mwandishi joel nanauka ambayo inaweza kukusaidia kupanga malengo yako vizuri na pia inasaidia kufanya tafakari vizuri kila wiki juu ya malengo yako.
Kikweli hii work book ilinisaidia sana, unajua kiukweli kitendo cha kujiwekea malengo na kuyaishi malengo yako inahitaji msaada wa hali ya juu na msaada wenyewe nakuomba utafute hii work book utaona matokeo yake.
naamini isingelikuwa kuwa na hii work book labda hata lengo langu la kuwa mwandishi lingekuwa lishafifia kwa hali ya juu sana lakini kutokana na hii work book imenisaidia kwa kiasi chake.
Gharama ya hii work book ni shilingi 10000 lakini msaada unaotokana na hii work book ni zaidi ya 10000 unayotoa.
na hii ndio ilikuwa silaha yangu mwaka uliopita na naenda kuitumia mwaka huu nakusihi na wewe ndugu yangu utumie.
19/12/2018
SILAHA YA PILI. .2018/2019...notebook.
Baada ya jana kuona silaha ya 1 ambayo ilikuwa ni diary leo naomba tuendelee na silaha ya pili.
Unajua unaweza ukawa na bunduki unataka kutumia k**a fimbo kiukweli hautaweza kuona faida ya hiyo bunduki bali utaona ni k**a mzigo kwako.
Hivi ndivyo ilivyo kwenye matumizi ya notebook.
Nakuomba k**a unataka notebook ikusaidie kwenye kutimiza malengo yako kwanza kabla ya kununua naomba ujiulize ni nini kitakacho kwenda kuijaza notebook yako.
MFANO:
1.Utanunua notebook kwa ajiri ya kuandika mawazo yako ya biashara tu. (hapa utahakikisha unaandika wazo lolote la biashara unalofikilia liwe dogo au liwe kubwa, liwe ni lako au umesikia sehemu wewe andika tu)
2.utaandika mawazo ya vitabu unavyopanga kuandika mwaka huu.
3.mawasiliano ya kila mteja kwenye biashara yako changa.
Kikweli ni vingi vya kuamua kuandika kwenye notebook yako.
Na ushauri wangu ni kwamba unaweza ukachagua vitu vya aina mbili ambavyo utakuwa unaandika kwenye notebook yako.
Lakini usiwe wakuandika kila kitu kwenye notebook yako. Sababu mwisho wa siku utahitaji kuipitia hiyo notebook yako sasa k**a ulikuwa unaandika kila kitu utaona hata uvivu kuwa unasoma maana itakuwa ni usumbufu.
Pia itachosha kusoma maana umeandikwa namba za rafiki zako, wazo la biashara, pia umeandika notes kidogo za shule au chuo, bado umeandika tarehe ya kifo cha bibi, bado umeandika nukuu za Aidan Mponeza.
Kiukweli huu utakuwa ni uchafu.
Hii ni silaha yangu mwaka uliopita na inaenda kuwa silaha yangu mwaka 2019.
Asante sana karibu kesho na mwendelezo wa silaha zingine.
©Aidan Mponeza
insta@aidanmponeza