17/01/2026
KESI 10 ZA MADAI AMBAZO HUTAKIWI KABISA KWENDA POLISI,
Bali ufuate utaratibu wa kisheria kupitia vyombo vya madai πUkikimbilia polisi kwenye suala la madai, unapoteza muda, unapoteza nguvu, na wakati mwingine unapoteza haki yako kabisa
βοΈ. Sheria haifanyi kazi kwa jazba wala kwa kelele, bali kwa utaratibu. Madai yanahitaji uthibitisho, nyaraka, na mamlaka sahihi ya kisheria. Polisi wanalinda maslahi ya jinai, si kugawa ardhi, si kulazimisha deni, si kupima mchango wa ndoa, wala si kuamua mirathi. Ukichanganya mamlaka, unajitengenezea vikwazo mwenyewe. Utaratibu sahihi si anasa, si upendeleo, wala si kuchelewesha haki. Ni ngao ya kisheria inayolinda madai yako dhidi ya dhuluma na matumizi mabaya ya madaraka. Mahak**a ipo kusikiliza, kupima, na kuamua kwa haki. Hapo ndipo madai yanapata thamani yake halisi ποΈ. Haki haipatikani kwa kukimbia, hupatikana kwa kufuata njia sahihi.
1. MIGOGORO YA ARDHI NA VIWANJA π‘
Hapa kinachoamuliwa ni umiliki, mipaka, au haki ya matumizi. Ni suala la nyaraka, ramani, ushahidi wa umiliki. π Hushughulikiwa na Baraza la Ardhi au Mahak**a. β Polisi hawagawanyi ardhi wala kuamua nani mmiliki halali.
Mahali pa kwenda Baraza la Ardhi la Kata, Baraza la Ardhi la Wilaya, au Mahak**a ya Ardhi kulingana na thamani na hatua ya shauri, Sheria zinazotumika,Sheria ya Ardhi,Sheria ya Ardhi ya Vijiji
Hapa kinachotazamwa ni umiliki halali, mipaka, na haki ya matumizi. Polisi hawana mamlaka ya kugawa au kufuta umiliki.
2. MIGOGORO YA NDOA NA MALI ZA NDOA π
Mgawanyo wa mali, madai ya mchango wa mke au mume, au haki baada ya kutengana. π Ni madai ya haki na usawa. β Polisi hawapimi mchango wa kupika, kulea watoto, au kushiriki ujenzi.
Mahali pa kwenda:
Bodi ya Usuluhishi wa Ndoa
Mahak**a ya Mwanzo au Mahak**a ya Wilaya
Sheria zinazotumika:
Sheria ya Ndoa
Mgawanyo wa mali, mchango wa wanandoa, na haki baada ya kutengana ni masuala ya madai, si jinai.
3. MIRATHI NA USIMAMIZI WA MALI YA MAREHEMU βοΈ
Nani arithi, kwa kiasi gani, na nani hana haki. π Mahak**a huamua kwa kuzingatia uhalali wa mirathi. β Polisi hawatoi urithi wala hawateui msimamizi wa mali.
Mahali pa kwenda:
Mahak**a ya Mwanzo, Wilaya, au Mahak**a Kuu kulingana na thamani ya mali.
Sheria zinazotumika:
Sheria ya Mirathi
Sheria ya Usimamizi wa Mirathi
Sheria za Kimila au Kiislamu pale inapohusika
Mirathi huamuliwa kwa nyaraka na sheria, si kwa makelele ya kifamilia.
4. MADENI YA KIBIASHARA AU YA KAWAIDA π°
Mtu amekukopa na hajalipa. π Hili ni dai la madai, linahitaji uthibitisho na uamuzi wa Mahak**a. β Polisi hawalazimishi ulipaji wa deni bila amri ya Mahak**a.
Mahali pa kwenda:
Mahak**a ya Mwanzo au Mahak**a ya Wilaya, Mahak**a ya Hakimu mkazi, na mahak**a kuu
Sheria zinazotumika:
Sheria ya Mikataba
Deni halibadiliki kuwa kosa la jinai kwa sababu tu mtu hajalipa.
5. MIGOGORO YA MIKATABA π
Uvunjaji wa mkataba wa ujenzi, upangaji, mauziano, au huduma. π Suluhisho ni madai ya kimahak**a au usuluhishi. β Polisi hawasimamii utekelezaji wa mikataba.
Mahali pa kwenda:
Mahak**a husika au Usuluhishi k**a mkataba umeelekeza hivyo.
Sheria zinazotumika:
Sheria ya Mikataba
Mahak**a huangalia makubaliano, masharti, na ukiukwaji wake.
6. MIGOGORO YA WAPANGAJI NA WENYE NYUMBA π
Kodi, kufukuzwa, au marekebisho ya nyumba. π Ni haki na wajibu wa kimkataba. β Polisi hawatoi amri ya kufukuza mpangaji wala kumrudisha ndani ya nyumba.
Mahali pa kwenda:
Baraza la Ardhi la kata
Sheria zinazotumika:
Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999
Hakuna kufukuza mpangaji kwa nguvu bila kufuata utaratibu wa kisheria.
7. MIGOGORO YA USHIRIKA AU UBIA WA BIASHARA π€
Faida, hasara, mgawanyo wa mapato, au uongozi. π Inahitaji hesabu, mikataba, na ushahidi wa kimaandishi. β Polisi hawatatui mgogoro wa faida kwa maelezo ya mdomo.
Mahali pa kwenda:
Mahak**a ya Biashara au Mahak**a ya Wilaya
Sheria zinazotumika:
Sheria ya Majina ya biashara
Sheria ya makampuni
Sheria ya Mikataba
Faida na hasara hugawanywa kwa mujibu wa makubaliano, si kwa shinikizo.
8. MADAI YA FIDIA (COMPENSATION) π
Ajali, uzembe, au hasara ya mali. π Kinachotafutwa ni fidia, si adhabu. β Polisi hawahukumu kiasi cha fidia.
Mahali pa kwenda: Mahak**a ya Mwanzo au Wilaya au hakimu mkazi au mahak**a kuu
Sheria zinazotumika: Sheria ya mwenendo wa madai Sheria ya Mikataba pale inapohusika
Lengo ni fidia, si adhabu.
9. MIGOGORO YA AJIRA NA KAZI π·
Mshahara, kufukuzwa kazi, mafao. π Kuna utaratibu maalum wa kisheria unaoheshimu haki za pande zote. β Polisi hawarudishi mtu kazini wala kuamuru mshahara ulipwe.
Mahali pa kwenda:
Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wa Migogoro ya Kazi
Sheria zinazotumika:
Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini
Mshahara, mafao, na kufukuzwa kazi havitatuliwi kituoni.
10. MIGOGORO YA KIFAMILIA ISIYO YA JINAI π¨βπ©βπ§
Msaada wa mtoto, malezi, au makubaliano ya kifamilia. π Hutatuliwa kwa madai au usuluhishi. β Polisi hawatatui haki za malezi kwa kufungana.
Mahali pa kwenda:
Baraza la Ustawi wa Jamii
Mahak**a ya Mwanzo, mahak**a ya wilaya
Sheria zinazotumika:
Sheria ya Mtoto
Maslahi ya mtoto ndiyo msingi, si hasira za wazazi.
TAFAKARI Polisi wanashughulika na makosa ya jinai tuuπ Mahak**a hulinda haki za madai βοΈ
Kabla ya kwenda polisi, jiulize k**a unatafuta adhabu au haki ya madai. Ukipata jibu sahihi, utajua mlango sahihi wa kugonga.
imendikwa na
Baraka Asajile Gwakabake (advocate)
0784745645
share na wengine au wataje rafiki zako waje wasome tujifunze wote
School Base-Online