OMIYO _AFRICAN QUEEN (ACCOUSTIC HAYA Version) Download FULl👉🏿https://youtu.be/wAfm2UAkXoI
Elimu Plus+
We offer the following:
2.Private proffessional examiners through IQUE-EXAMS.
3.Secretarial Services
WELLCOME
17/02/2022
"Furaha ndo kilele cha mafanikio kwa mwanadamu"
24/01/2022
Ukimuona toa taarifa🙏🏿
01/12/2021
TASWIRA YA MHITIMU KWA
WAZAZI/JAMII YETU
Msomi_aliyepoteza_Funguo_Mtaani✍️
Na Ediga Mushobozi
Kwanza.
Wazazi wengi wa kiafrika wamerithi imani fulani japo sijui kutoka wapi. Wazazi wote na jamii ya Kiafrika kwa ujumla wanaamini kuwa ili kijana aonekane amesoma na elimu imemsaidia lazima apate ajira serikalini. Wanashindwa kutafakari kuwa msomi ni mtu aliyejikomboa kifikra ana uwezo mkubwa wa kuwaza na kuibadili jamii, pia ana uwezo mkubwa wa kujiajiri na kutangeneza ajira nyingi kwa vijana wenzake wasiosoma na jamii anamoishi. Pia pamoja na ajira serikalini kuna ajira za mashirika, makampuni viwanda nk.
Pili.
Wazazi / Jamii zetu za kiafrika zina kasumba ya kumponda, kumshusha na kumkandamiza msomi asiyeajiliwa serikalini baada ya kushirikiana naye ili aweze kuwapa mawazo chanya yenye kuleta mabadiliko katika jamii husika. Kumbuka Msomi ni lulu. Msomi ni mali. Msomi ni hazina ya jamii anakotoka na Msomi ana nguvu kubwa ya kuibadilisha jamii kimawazo na kiuchumi. Yani anaposoma kijana mmoja ndani ya jamii fulani basi tunaamini Vijana kumi(10) katika ile jamii nao wamesoma kupitia yeye....
Tatu,
Wasomi wengi pia wamelala sana ndo maana hata jamii wakati mwingine haioni effect yao. Kwasababu pamoja na yote hayo msomi anatakiwa kuwa tofauti na vijana wengine. Kwanza maana ya kuwa somi hutakiwi kutetereka, hutakiwa kukata ama kukatishwa tamaa maana k**a umeweza kuvumilia changamoto zote za shuleni hadi umefanikiwa kuhitimu tunaamini hakuna kitu cha kukuondoa kwenye reli baada kutudi mtaani.
Lakini pia
Msomi leo baada ya kurudi mtaani kubadilisha jamii anarudi na kuanza kuungana na vijana Wavuta bangi, anashinda vijiweni na stori za majungu, anakuwa mlevi wa pombe za kinyeji. Sasa kwanini jamii isikutukane na kukudidimiza?
Nne..
Msomi inabidi ujibrand. Sio kwamba ujidai ili jitengenezee mazingira ya kuheshimika kwenye jamii kuanzia maongezi (mawazo chanya na mapya) mavazi, na mienendo kwa ujumla.....
Itaendelea kwenye kitabu cha ALIYEPOTEZA FUNGUO MTAANI
25/11/2021
USHAURI WA BURE KWA VIJANA WASOMI (WAHITIMU) na Mushobozi.
1. Tunaamini Vijana wengi tunatoka familia duni na za Vijijini. Wakati mwingine kula milo miwili katika familia zetu ni tatizo.
2. Unapobahatika kupata nafasi ya kuendelea kimasomo jicho la mzazi linaanza kukutazama k**a mkombozi wa familia yenu. Hapo mzazi/wazazi hujitoa kwa kila kitu ikiwemo kuuza kuku, mbuzi, bata na mashamba lengo ni usome upate kazi ili uwainue wadogo wako na familia kwa ujumla.
3. Unakuta kijana anapata nafasi ya kwenda chuoni huku akiwa amebebeshwa mzigo wa matatizo yote ya familia yake.
4. Ila vijana wengi wakishafika vyuoni mizigo ya familia zao wanazitua chini na kuanza kuiga maisha ya vijana wengine ambao wakati mwingine hujui wao wanatoka familia ya namna gani, basi mnakuwa watu wa club, pombe, mademu/wanaume, iphone, na mwishowe vijana unaanza kukabiliwa na (SUP) za kutosha na mawazo yako yanakuwa ya ulimbukeni, na mwishowe wengine wanashindwa kuendelea na masomo (disco) na wanaobahatika wanamaliza chuo wakiwa na iphone 7, techno, infinix na G.P.A ya 2.5 huku kichwa kikiwa kina ziro kuhusu elimu ya mtaani.
4. Unarudi mtaani (Kijijini/mjini) ambako maisha yako yote yatakuwa huko (street) ukiachana na maisha ya mda ya chuo ya miaka mitatu, unaanza kusambaza barua za ajira mwishowe ajira hupati kwasababu waliohitimu mtaani ni wengi sana. Na ukibahatika unapata ajira za mateso (mshahara laki na nusu/laki mbili) na wakati mwingine hupati kwa wakati.
5. Hapo kumbuka wazazi wanakutegemea k**a mkombozi wao ajira serikalini ni finyu. Mwishowe na umri umesogea. Unaonekana mzigo katika familia mpaka wazazi wanaanza kukuchukia maana umekula kila walichokuwa nacho hujarudisha chochote na jembe ushasahau kushika ama hutaki kazi za shambani zinakuchafua.
6. Unaamua kwenda mjini kutafuta kazi na mjini ndo kuna hatari zaidi. Unatoa maamuzi ya kuishi dukani kwa muhindi huku (UNAOMBA KUFANYA KAZI YOYOTE) ilimradi mkono uingie kinywani huku familia yako kijijini inateketea na wewe umri unasogea 40's kwasababu umekaa shuleni miaka 23 na umehitimu ukiwa na miaka 30.
USHAURI
1. UNDA VIKUNDI
Vijana jifunze kutengeneza umoja mkiwa chuoni na baada ya kumaliza vyuo na kujenga mipango thabiti ya kushirikiana kwa kujijenga kiuchumi na Kwa kujiajili. Mkishakuwa na vikundi weka mikakati, andika miradi bunifu, sajilia vikundi vyenu katika ofisi za afisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata na wilaya, omba mikopo kutoka kwenye mifuko ya maendeleo ya vijana akina mama na wazee, JIAJILI kwa kuendesha miradi yenu.
Itaendelea...................
16/10/2021
"Usilazimishe kulipwa fadhila kupitia mgongo wa msaada wako"✍️
By - Ediga Mushobozi
The Wizard of Bongo flavour is here with this tune 💔
Link his youtube bio
💔 AUDIO OUT NOW🎹
produced by🎹
Md_production🎧
13/09/2021
The Wizard of Bongo flavour is here with this tune 💔
Link his youtube bio
💔 AUDIO OUT NOW🎹
produced by🎹
Md_production🎧
07/09/2021
"Kila raheli Darasa la Saba"
The super talented Omiyo De Jinn
Anakukaribisha kutizama video yake mpya
Naanzaje - (Cover) by plutnumz
Link his bio for full video
28/08/2021
The super talented Omiyo De Jinn
Anakukaribisha kutizama video yake mpya
Naanzaje - (Cover) by plutnumz
Link his bio for full video
24/08/2021
"Matajiri wataendelea kuwa matajiri zaidi kwasababu maskini wamejawa woga huku wakidhani kila fursa ni utapeli"
By - Ediga Mushobozi
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the school
Telephone
Website
Address
Kongowe Mbagala Near Street Matthew's Pre And Primary School
Dar Es Salaam