Elizabeth David

Elizabeth David

Share

Mwalimu, Mwandishi na Mshauri Pokea mafundisho upate uzima

25/08/2025

HAKUNA MKAMILIFU .

Rehema za Mungu ni mpya kila siku asubuhi. Mungu alichungulia kutoka Mbinguni akaona ya kuwa wanadamu wote wamemkosea. ashukuriwe Yesu aliyejitoa kwa ajili yetu, msamaha wa uovu wetu wote aliuondoa nakuupeleka pale msalabani.
Ndugu yangu mpendwa wangu, usijiue kwa kujiona kuwa ni mkosaji, badala yake, Yesu anakuita anasema njoo, njoo ulivyo, lete masikitiko yako, lete hasira yako, lete uchungu wako, lete mizigo yote kwangu. Njoo ujifunze kwangu, kwa maana mzigo wangu ni mwepesi na nira yangu ni laini. huyo ni Yesu.
Ninaposema hakuna mkamilifu duniani ila Mungu namaanisha katika mambo yote. tunakuwa wakamilifu kupitia Yesu , tunapata haki ya ukamilifu kwa sababu ya Yesu.
Ilinichukua muda mrefu sana kujua urahisi wa kumtwika Mungu fadhaa zangu, na kupeleka mizigo yangu kwa Yesu. ijapokuwa kila siku naenda kanisani, najifunza, bado sikujua namna gani nitaachilia mizigo niliyoibeba , ili nipate utulivu wa nafsi, amani moyoni.
Najua unajiuliza jinsi gani sasa nitafikia huko. Usiogope.
Kumbuka hili neno moja kwanza. USIJISUMBUE KWA NENO LOLOTE, BALI KATIKA KILA NENO, KUOMBA, KUSALI NA KUSHUKURU, NA HAJA YA MOYO WAKO IJULIKANE MBELE ZA MUNGU.
Si unajua kuwa neno la Mungu linayatambua mawazo ya moyo wako?, tena basi hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake.
Mungu anasema , kabla hujaomba amekujibu, zaidi anasema , unapokuwa katika kuomba, anasikia.
Sasa wewe fanya bidii kumtafuta,
amesema omba utapewa, tafuta utaona, bisha, atakufungulia mlango wako., anaendelea kusema niite tu nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa magumu, usiyoyajua.
Mungu anakuwazia mema wala sio mabaya , ili upate tumaini katika maisha yako.
Mtafute basi kwa moyo wako wote, kwa akili zako, zote kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote . Weka UPENDO katika hayo yote, nawe utamwona, ataonekana live.
Ni kwa msaada wa Mungu pekee, tunaweza kuwa wakamilifu katika Kristo Yesu. tambua hili nalo kuwa hakuna mtu anaweza kwenda kwa Yesu bila ya kuvutwa na Mungu. yote yanawezekana kwa Mungu Baba.
Hakuna lisilowezekana kwa Mungu.
Kumbuka huu mfano wa Yesu, kwamba ni rahisi ngamia kupenya katika tundu la Sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa Mungu.
Maana yake nini . kwa mwanadamu ni vigumu lakini kwa Mungu inawezekana.. amini kuwa Yesu anakupenda. sema tu . Amen.

17/08/2025

MAISHA NA KWELI YAKE
Lakini mkiitimiza Ile Sheria ya kifalme, Ile ya kumpenda jirani yako k**a nafsi yako, hamko chini ya Sheria.
Basi mwanadamu wa Tabia ya asili hawezi kutambua mambo haya ya rohoni , mana kwake ni upuuzi Kwa kuwa hayafahamu mambo ya Mungu.
Lakini mtu wa Rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.
Lakini pia tambua kuwa unapowapa watu muda wako na umuhimu wako, wanafikiri kuwa huna la kufanya. Wanafikiri watakupata muda wrote , wanasahau kuwa wewe ndio umetafuta muda na kukusanya nguvu ya kuwa pamoja nao.
Siku zote maishani tambua kuwa ulimi hauna mfupa, lakini Una nguvu ya kutosheleza kuvunja moyo wa mtu. Kwa hio kuwa makini na maneno yako muda wote. Kwa kila neno unaloongea litapimwa, utahukumiwa kwa maneno yako sio matendo..
Duniani humu, hakuna kitu kinachodumu milele . Usijipe presha Kwa Jambo lolote. Yesu amesema leteni mizigo yenu mizito, Nira ngumu ili abadilishe , kujipatia wepesi wa mizigo na nira nzito ni kumfahamu Yesu na kumpenda, kulipenda neno lake na kulishika.
Haijalishi unapitia hali ngumu kiasi gani. Itabadilika tu.
Asubuhi yako lazima ije, hata k**a usiku ni mrefu kiasi gani.
Kumbuka, wakati mwingine Mungu huwa anakata Majani mbele yako ili uweze kumuona nyoka.
Ambatana na watu ambao wanaona fahari kuwa nawe, wanakujali, wanakuheshimu, na kukupenda pasipo na sababu yeyote. Jinsi ulivyo.
Maisha ni mapambano. Lakini ukiwa na Yesu anakusaidia ili ujisikie Raha nafsini mwako, hekima ya kukuwezesha kifanya mambo Kwa wepesi na ufasaha mkubwa.
Unapokuwa nacho furahi na ukikosa FIKIRI.
Mungu anakupenda.

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00